Natural Resources Canada logo and Government of Canada logo
Symbole du gouvernement du Canada
Kuyapa nguvu Maamuzi ya Nishati safi

Muhtasari Mkuu

Kituo cha kufanya maamuzi na msaada wa nishati safi cha RETScreen kinatafuta kujenga uwezo kwa waandaaji, watoa maamuzi na viwanda kufanya miradi ya nishati za kujadidika na ufanisi wa nishati. Dhumuni hili linafanikiwa kupitia: kuendeleza nyenzo za kufanya maamuzi (k.m. softiweya ya RETScreen) ambayo unapunguza gharama za tafiti za awali za kuangalia uwezekano; kusambaza ujuzi wa kusaidia watu kufanya maamuzi sahihi' na kwa kufundisha watu kuchanganua vyema masuala ya fedha na ufundi kwa miradi inayowezekana.

Softweya ya RETScreen ya Kuchambua Miradi Safi ya Kuchambua Miradi Safi ya Nishati ni ya aina yake katika kufanya maamuzi iliyotayarishwa kwa michango ya wataalamu mbalimbali kutoka serikalini, viwandani na katika taasisi za elimu. Softweya , inayotolewa bila malipo, inaweza kutumika sehemu yoyote ulimwenguni kutathmini uzalishaji wa nishati, uhifadhi, gharama, upunguzaji wa utoaji hewa iharibuyo mazingira, ufaaji kiuchumi na hatari kwa matumizi ya aina mbalimbali za nishati jadidifu na teknolojia za ufanisi katika matumizi ya nishati. Softweya (inayopatikana katika lugha mbalimbali) pia inahusisha bidhaa, miradi, rasilimali maji, na takwimu za hali ya hewa, mwongozo wa mtumiaji, na mifano ya matumizi kutoka kozi za viwango vya vyuo vikuu pamoja na kitabu cha kielektroniki cha uhandisi.

RETScreen ya kimataifa ina simamiwa chini ya uongozi na msaada wa kifedha wa kituo cha utafiti cha CanmetENERGY. cha Rasilimali ya (NRCan), ya Kanada. RETScreen imetengenezwa kwa ushirikiano wa serikali mbalimbali na mashirika ya kimataifa, na msaada wa kitaalamu kutoka katika mtandao mkubwa wa wataalamu kutoka viwandani, serikalini na taasisi za elimu.

Bonyeza hapa ili kupakua bure RETScreen 4 (44 MB).