Natural Resources Canada logo and Government of Canada logo
Symbole du gouvernement du Canada
Kuyapa nguvu Maamuzi ya Nishati safi

Pakua Bure

Softweya ya RETScreen ya Kuchambua Miradi Safi ya Nishati ni ya aina yake katika kufanya maamuzi iliyotayarishwa kwa michango ya wataalamu mbalimbali kutoka serikalini, viwandani na katika taasisi za elimu. Softweya , inayotolewa bila malipo, inaweza kutumika sehemu yoyote ulimwenguni kutathmini uzalishaji wa nishati, uhifadhi, gharama, upunguzaji wa utoaji hewa iharibuyo mazingira, ufaaji kiuchumi na hatari kwa matumizi ya aina mbalimbali za nishati jadidifu na teknolojia za ufanisi katika matumizi ya nishati. Softweya (inayopatikana katika lugha mbalimbali) pia inahusisha bidhaa, miradi, rasilimali maji, na takwimu za hali ya hewa, mwongozo wa mtumiaji, na mifano ya matumizi kutoka kozi za viwango vya vyuo vikuu pamoja na kitabu cha kielektroniki cha uhandisi.

Bonyeza hapa ili kupakua bure RETScreen 4 (44 MB).

Programu na Mahitaji ya Data: Microsoft® Excel 2000 au juu zaidi; Microsoft® Windows 2000 au juu zaidi; na Microsoft .NET Framework 2.0 au juu zaidi. Tafadhali hakikisha kwamba visasisho vipya kutoka kwa Microsoft (www.microsoft.com) vya Windows na Excel zimesakinishwa kwenye kompyuta yako.