Natural Resources Canada logo and Government of Canada logo
Symbole du gouvernement du Canada
Kuyapa nguvu Maamuzi ya Nishati safi
RETScreen ni nini?

Bofya hapa kupakua *.pdf (1.76 MB)


RETScreen® International
www.retscreen.net

Softweya ya RETSreen ya Uchunguzi wa  Projekti ya Nguvu Safi
Softweya ya RETSreen ya Uchunguzi wa Projekti ya Nguvu Safi ni softweya inayo ongoza ulimwenguni ya-kuafikia maamuzi ya nguvu safi. Inatolewa bila malipo yoyote na Serikali ya Canada kama sehemu ya utambuzi wa Canada wa mahitaji ya kuchukua hatua za kuunganisha ili kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa na kupunguza uchafu. RETScreen ni thibitisho kinachowezesha miradi ya nguvu safi ulimwenguni kote.

RETScreen inapunguza gharama kwa kiasi kikubwa sana (kifedha na muda) zinazo husiana na kutambua na kukadiria uwezekano wa miradi ya nguvu. Gharama hizi, zinazotokea wakati wa hatua za kabla ya uwezekano, uwezekano, maendeleo, na hatua za uhandisi, zinaweza kuwa vipingamizi vikubwa kwa maendeleo ya Nguvu zinazoweza kurudiwa upya na Teknolojia za Ufanisi-nguvu. Kwa kusaidia kuanisha vipingamizi hivi, RETScreen inapunguza gharama ya kuanzisha miradi na kufanya biashara katika nguvu safi.

RETScreen inaruhusu waamuzi na weledi kuamua kama pendekezo ya nguvu inayoweza kurudiwa upya, ufanisi wa nguvu, au mradi wa utoaji pamoja wa nguvu inaleta maana kifedha. Ikiwa mradi unaweza kutekelezwa-au kama hautekelezwi-RETScreen itamsadia mwamuzi kuelewa yafuatayo: haraka, kwa kauli moja, katika muundo wa matumizi-mazuri, na gharama ndogo kabisa

RETScreen:
  • Inatumiwa na zaidi ya watu 425,000 katika nchi na maeneo 222
  • Inapatikana katika lugha 35 zinazo enea zaidi ya 2/3 ya watu wa ulimwengu
  • Sehemu ya muhtasari katika zaidi ya vyuo vikuu na vyuo 600 ulimwenguni kote.

RETScreen inahusika moja kwa moja na uokoaji wa matumizi ya zaidi ya $7 bilioni ulimwenguni kote, nambari inayotarajiwa kukua na kufikia zaidi ya $8 bilioni ifikapo 2013. Kwa sababu ya kuwezesha nguvu safi, RETScreen inachangia kwa njia isiyo dhahiri upunguzaji mkubwa katika utoaji wa gesi katika nyumba za vioo-upunguzaji unaokaridiwa kuwa tani milioni 20 kila mwaka ifikapo mwaka 2013. Na ifikapo mwaka 2013, inakadiriwa kuwa RETScreen itakuwa imeshasaidia msukumo wa kuanzisha angalau uwezo wa GW 24 wa nguvu safi ulimwenguni kote ikiwa na thamani ya $41 bilioni.


Hatua Tano za Kiwango cha Uchanganuzi
Softweya na Data

RETScreen ni bidhaa pekee ya aina yake inayo fahamika, inayowaruhusu wahandisi, wasanifu, na wapangaji kifedha kuigiza na kuchanganua mradi wowote unao husika na nguvu safi. Waamuzi wanaweza kuendesha uchanganuzi wa hatua tano za vipimo ukijumuisha uchanganuzi wa nguvu, uchanganuzi wa gharama, uchanganuzi wa utoaji gesi, uchanganuzi wa kifedha na uchanganuzi wa unyeti/hali ya hatari.

Teknolojia zinazo patikana katika modeli ya mradi wa RETScreen zinajumuisha zote pamoja, na zinajumuisha vifaa vya desturi na visivyo vya desturi vya nguvu safi pamoja na vifaa vya kawaida vya nguvu safi na teknolojia. Sampuli ya modeli za mradi inajumuisha: ufanisi nguvu (kutoka vifaa vikubwahadi nyumba za watu binafsi), kupasha joto na kupoza, (kwa mfano,mkusanyiko wa viumbe hai, pampu za joto, na upashaji joto kwa kutumia mionzi ya jua/upashaji maji) nguvu (ikijumuisha vifaa vya kufanywa upya , upepo, mawimbi, haidrona n.k. lakini vile vile teknolojia za kawaida kama vile tabo za gesi/mvuke na injini zinazo rudishiana) , najoto na nguvu zinazotumika pamoja (au uzalishaji nguvu pamoja)

Seti ya kumbukumbu za data Zilizounganishwa
Zinazo unganishwa pamoja katika vyombo hivi vya uchanganuzi ni kumbukumbu la data za bidhaa, mradi, haidrolojia (ya mwisho ikiwa na 6,700 kituo cha ardhini pamojana NASAdeta za satilaiti ambazo zinafunika sehemu zote ulimwenguni), pamoja na uunganishaji na ramani za vifaa vya nguvu ulimwenguni kote. Na ili kumsaidia mtumiaji haraka kuweza kuanza uchanganuzi, RETScreen imejengea ndani kumbukumbu la data kubwa sana ya violezo vya miradi ya nguvu safi

Hakuna chombo kingine kinachosaidia kuendesha uchanganuzi mkubwa.


Mafunzo

Mafunzo ni sehemu muhimu ya RETScreen. Inayopatikana ndani ya softweya iliyopakuliwa au utandawazi ni mafunzo yasiyo na malipo yakitofautiana kwa urefu kutoka mhadhara mmoja mpaka kozi za siku kadhaa. Ikijumuishwa pamoja, violezo vya mafunzo vinatosha kuendeshwa kwa kozi za makini za wiki 2-4 au kozi za kawaida za muhula 1-2 Inayojumuishwa na vifaa vya mafunzo ni:
  • matangazo makini ya utandawazi,slaidi za utoaji, na kumbukumbu za mwalimu;
  • uchunguzi kifani kadhaa ikiwa ni pamoja na kazi za nyumbani utatuzi uliokwisha fanyika , na taarifa kuhusu jinsi miradi ilivyotekelezwa katika mazingira halisi
  • kitabu cha utondoti cha mtumiaji
  • kitabu cha kiada kinachotoa maelezo ya utondoti ya
  • Kisanduku cha Vifaa vya Kisheria cha Nguvu Safi

Wabia

Njia za kukuza za RETScreen zimetoa mfano bora wa ushirikiano wa kimataifa unaofanikiwa RETScreen imeanzishwa na kudumishwa na serikali ya Canada kupitia Mali Asili ya Canadaya CanmetENERGY kiituo cha utafiti Verennes, Quebec na inasaidiwa na mfumo wa kimataifa wa wataalam kutoka viwanda, serikali na taaluma Wabia wakuu wanajumlisha Utawala wa Kitaifa wa Ndege na Anga (NASA), Nguvu Zinazorudiwa Upya na Ubia wa Ufanisi wa Nguvu (REEEP),Shirika la Umoja wa Kimataifa la Programu ya Mazingira (UNEP) na Kifaa cha Ulimwengu cha Mazingira (GEF).

Wabia
Mwisho

Pamoja na RETScreen, Canada inaongoza katika uendelezaji wa teknolojia ya nguvu safi-sehemu muhimu sana ya vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Ikitambuliwa kimataifa kwa ajili ya mafanikio yake maalum, RETScreen inapanuka na kutia nguvu soko la ulimwengu la teknolojia za nguvu zinazorudiwa upya, ikitia moyo utekelezaji hatua za ufanisi za nguvu, na kuchangia upatikanaji wa nguvu za kudumu za siku za baadaye. Jinsi dunia inavyoelekea upande wa kulikabiliana na swala la mabadiliko ya hali ya hewa na kulinda mazingira, Canada inadhamiria kusaidia kuongoza jitihada nchini na ng'ambo. RETScreen inaweza na itakuwa na athari kubwa ya kujenga sekta ya nguvu safi ulimwenguni

Tunakuhimiza upakue softweya kutoka kwenye mtandao wetu na upate uzoefu wewe mwenyewe wa nguvu ya RETScreen. Na kama umekubaliana na manufaa ya softweya yetu, tafadhali zungumza kuhusu RETScreen na marafiki na wafanyakazi wenzako.